TUNAOMBA RADHI SANA WAPENZI WASOMAJI NA WATIZAMAJI KATIKA TAARIFA HII KWA PICHA ZA KUTISHA.
Dereva
wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka
sasa (kwani hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu
wake wa kulia mara baada ya kugongwa na roli la mchanga katika eneo la
daraja la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa
mujibu wa Mwandishi wa G. Sengo Blog Peter Fabian aliyeweza kuwahi
kufika eneo la tukio na kutoa msaada wa gari kumfikisha dereva wa
pikipiki hiyo aliyopata ajali Hospitali ya Rufaa ya Bugando, annasema
kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Mkolani kuelekea Buhongwa na Roli hilo
lilikuwa likitokea Buhongwa kuelekea Mkolani, imetokea wakati dereva wa
roli 'akiovateki' daladala iliyokuwa mbele yake ikibeba abilia, hivyo
alipoipita tu daladala hiyo akakutana uso kwa uso na bodaboda.Baadhi ya bodaboda na wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD Kanda ya Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.
Sambamba na kuvunjika mguu pia dereva huyo amevunjika vidole vitatu vya mkono wake wa kulia. |
NA: PETER FABIAN
SOURCE: GSENGO.
No comments:
Post a Comment