Thursday, 28 November 2013

KOMBE LA DUNIA KUTUA MWANZA KWA MARA YA KWANZA, KUWEKA HISTORIA.

Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia litapokelewa Mkoani Mwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, mbele ya waandishi wa habari na kamati ya maandalizi ya ujio huo katika ukumbi wa Mwanza Hotel hivi leo.
 
Ndikilo amesema hii ni mara ya kwanza kwa kombe hilo kupokelewa katika Mkoa huo na akawataka wanachi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kulipokea,amesema na kuongeza kuwa "Mhe shimiwa Rais ambaye yupo ziarani katika Mkoa wa Simiyu amekubali kulilaki kombe hilo katika mkoa wetu wa Mwanza hii ni heshima kubwa kama wananchi wa Mkoa huu na wapenda michezo kwa ujumla.
 
Amesema kombe hilo litawasili katika uwanja wa ndege wa mwanza majira ya saa tatu asubuhi na badae kupelekwa katika uwanja wa CCM Kirumba, ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya wananchi watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Coca Cola Nchini bw. Eyebolt Gretchen, amesema ujio wa Kombe hilo kwa mara ya tatu katika nchi ya Tanzania nia pamoja na amani ya nchi iliyopo na ukarimu wa watu wake, Miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimekuwa na utulivu hata kufanya kutembelewa na kombe la Dunia ni Tanzania, amesema na kuongeza kwamba, kama Coca cola wamekuwa mstari wa mbele kwenye jitihada za kukuza soka nchini ikiwapo mashindano ya Kopa Coca cola.
 
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu amewahakikishia wanachi wote wa Mkoa wa Mwanza amani na utulivu, aidha amewaomba wananchi kutokuja wanjani hapo wakiwa na watoto wadogo ili kuepusha adha wanayoweza kupata watoto hao" Labda niombe ndugu zangu kwa wale watoto wadogo ni vema wakaachwa nyumbani kuepuka usumbufu". alisema na kuongeza kuwa watu hawataruhusiwa kusogea karibu na eneo la Pitch ya uwanja huo.
 
Hii ni mara ya tatu kombe hilo linakuja hapa nchini ambapo mara zote limekuwa likipokelewa na kulakiwa na wananchi waishio katika Mkoa wa Dar es Salaam. 
 
Wadadisi wa mambo wanasema kwamba, ujio wa kombe hilo si tu kwamba linakuja kutazamwa na wanachi wa Mwanza bali pia ni frsa nzuri kwa mkoa huo kujitangaza kimataifa lakini pia kutangaza rasilimali zinazo patikana katika Mkoa huo alkini pia iwe chachu kwa vingozi kuona kuna umuhimu wa kuipa kipaumbele michezo yote, anasema Mashaka Baltazari mwandishi mwandamizi wa Jambo Leo na Mwakilishi Mkoani Mwanza.

SOURCE: AFISA HABARI MKOA
                  MWANZA.
 

Tuesday, 26 November 2013

Wananchi ‘wawashtaki’ viongozi kwa mbunge

Wasema hawachukui hatua za kushughulikia kero zinazowakabili kwa muda mrefu
Wananchi  wa Mtaa wa Mwanzomgumu katika Kata ya Bigwa,  Manispaa ya Morogoro, wamewashtaki kwa mbunge wa jimbo hilo, Abdullaziz Abood, viongozi wa serikali ya mtaa huo, kwa kile walichokielezea kuwa ni kushindwa kuwatumikia.
Wananchi hao walisema tatizo hilo pia liko katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ambayo haifanyi jitihada za kutosha, ili kuwaondolea kero mbalimbali zikiwemo kukosa baadhi ya huduma muhimu.
Abood alipita katika mtaa huo akiwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa Kata za Bigwa, Mindu na Mkundi ambapo pia alikabidhi  vifaa mbalimbali.
 Msaada wa vifaa hivyo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake za wakati wa kampeni  za uchaguzi wa mwaka 2010, ni pamoja na  vyerehani, mabomba ya kusambazia maji, mawe, kokoto, mifuko ya saruji, mchanga na hundi za fedha.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, wananchi wa Mtaa Mwanzomgumu, walisimamisha msafara wa mbunge Abood na  kumlalamikia kitendo cha viongozi wao kutowajali kwa maana ya kushughulikia kero zao.
Wananchi hao walisema eneo lao linakabiliwa na matatizo mengi, lakini viongozi wao hawafanyi jitihada za kupunguza kama si kumaliza kabisa matatizo hayo.
Walisema matatizo hayo ni pamoja na ubovu wa barabara, kutozwa Sh100 kwa kila ndoo ya maji, ili kuchangia huduma hiyo na kukosekana kwa kituo cha polisi.
Baada ya malalamiko hayo, Abood aliwaita viongozi wa eneo hilo ili wajadiliane naye kuhusu namna ya kutatua matatizo hayo, lakini waligoma.
Badala yake, walimtaka aende walikokuwa, lakini naye alikataa kwa sababu ratiba ya ziara yake ilimbana.

SOURCE: MWANANCHI.

Diwani amkosoa Lissu

Mwanasheria mkuu wa Chadema,Tundu Lissu. 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Novemba25  2013  saa 11:36 AM
 
Dar es Salaam. Wakili wa kujitegemea na Diwani wa Kata ya Mabogini mkoani Kilimanjaro (Chadema), Albert Msando ameeleza kasoro nne za kisheria ambazo zimefanywa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu wakati wa kutoa hukumu kwa makosa yaliyofanywa na makada wa chama hicho, Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msando alisema Katiba ya Chadema inaeleza kuwa kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi.
“Tunaomba Lissu aeleze kwa njia ileile aliyotumia kueleza umma wa Watanzania uamuzi wa Kamati Kuu, siku na tarehe ambayo Dk Kitila na Zitto walipewa mashtaka yao kwa maandishi na atoe nakala ya majibu yao kwa maandishi kama yapo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema,” alisema na kuongeza:
“Aeleze ni utaratibu gani ulitumika kuwajadili kwenye kikao cha Kamati Kuu, kufikia uamuzi na kuwapa adhabu ya kuwavua madaraka wakati hawajapewa mashtaka hayo kwa maandishi kama Katiba inavyosema, kisha Kamati Kuu kwenda kwenye vyombo vya habari na kueleza kuhusu uamuzi huo na kutoa siku 14 ili wajieleze.”
Alisema Lissu hatakiwi kutoa majibu ya jumla, bali kueleza utaratibu, sheria na utawala bora gani uliotumika kuchukua uamuzi huo dhidi ya Zitto na Dk Kitila. Alisema Lissu pia anatakiwa kueleza aina ya ushahidi alionao ambao ulitumika kuwahukumu.

SOURCE. MWANANCHI.

Monday, 25 November 2013

Rage ampinga Malinzi kweupe

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) katiba ya Simba katika mkutano alioufanya jana Jumapili kuhusu kusimamishwa kwake. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo, Barabara ya Msimbazi, Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga. 
Na Sosthenes Nyoni, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Novemba25  2013  saa 14:27 PM
 
Kwa ufupi
 
Awali, Rais wa TFF, Jamal Malinzi akizungumza na Wanahabari alimtaka Rage aitishe mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba ndani ya siku 14 kuanzia Novemba 23. 

Rage amemteua Wambura  kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba.
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage amepinga agizo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linalomtaka aitishe mkutano wa mabadiliko ya katiba ndani ya siku 14 na kusema endapo msimamo huo utasisitizwa basi atajiuzulu.
Awali, Rais wa TFF, Jamal Malinzi akizungumza na Wanahabari alimtaka Rage aitishe mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba ndani ya siku 14 kuanzia Novemba 23.
“Kutokana na Mgogoro uliopo Simba hivi sasa, kamati ya utendaji ya TFF inamwagiza mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kuitisha mkutano mkuu wa dharura ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
“Uamuzi huu umefanywa kwa kuzingatia ibara ya 1(6) ya katiba ya Simba inayosema Simba Sports Klabu ni mwanachama wa TFF, itaheshimu katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF,” alisema Malinzi.
Lakini jana mwenyekiti wa Simba, Rage akizungumzia agizo hilo la TFF alisema hawezi kuitisha mkutano huo kwa shinikizo la shirikisho hilo.
“Katiba ya TFF ibara 31(1-5) inasema mjumbe wa kamati ya utendaji atakosa sifa kama atakosa mambo manne, ataandika barua kujiuzulu, haudhurii mikutano minne iliyoitishwa na mwenyekiti  halali, kama atakuwa mgonjwa amelala kitandani miezi 12  mgonjwa na amekutwa na kosa la jinai,” alisema Rage.
Alisema,” nimesikitishwa na agizo la TFF kunitaka niitishe  mkutano ndani ya siku 14, wamenukuu ibara ya 1(6), Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, nitaheshimu katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF, hatuwezi kuheshimu kuvunja katiba ya TFF, mimi naambiwa nivunje katiba ya TFF naambiwa nivunje katiba ya Simba.”
“Tena wamekwenda mbali wananitaka niitishe mkutano ndani ya siku 14 sijui wameitoa wapi, haipo kwenye katiba ya TFF wala Simba, mimi msimamo wangu kama mwenyekiti wa Simba siitishi mkutano nalindwa na katiba,” alisema Rage.
Akizungumzia kamati ya utendaji iliyoketi na kumsimamisha, Rage alisema ilikuwa batili kutokana na kuongozwa na mtu ambaye hatambuliki katika katiba ya klabu yake ya Simba.
“Kamati ya utendaji ya Simba inakamilika kwa kuwa na mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe saba waliochaguliwa katika uchaguzi halali, hakuna  sehemu inayomtaja kaimu mwenyekiti au umewahi kuona wapi mtu ana kaimu na kukaimu, huyo Itangire si amewekwa tu pale, alichaguliwa na nani?” Alihoji Rage. Alijitapa kwa kusema hatua yake ya kwenda kuzunguza makao makuu ya klabu yake imedhihirisha yeye ndiye mwanaume wa kweli na aliwaponda wapinzani wake kwamba ni waoga kutokana na kumjadili mafichoni.
“Siku zote ukitaka kupindua nchi unaanza kuteka Ikulu, mimi ndiyo mwanaume wa kweli siyo hao wanaoongelea huko uchochoroni huo si uoga?” alijigamba Rage. 
 
 Katika hatua nyingine, Rage amemteua Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba na kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Rahma Al Kharoosi aliyejizulu kutokana na kutingwa na majukumu.
 
SOURSE: MWANANCHI. 

Zitto ajiweka njia panda

“Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?”  Dk Slaa. 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Jumanne,Novemba26  2013  saa 8:40 AM
 
Kwa ufupi

Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.
 
Dar es Salaam. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amejiweka katika mazingira magumu zaidi kisiasa ndani ya chama hicho, kutokana na shaka kubwa iliyougubika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam juzi.
Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.
Leo, uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
Miongoni mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa nyadhifa zao.
Mchange na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM wanakoendeleza harakati zao za kisiasa.
Jana, Machange alipotafutwa, alisema: “Mimi sikuwahi kuondoka Chadema, nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema nimeondoka.
Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu.
“Mimi ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote, walioondoka ni Mwampamba na Shonza.” Mwampamba alisema: “Nilijitokeza pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu.”
Kuwepo kwao katika mkutano wa Zitto kunaweza kutumiwa na uongozi wa Chadema kuwa uthibitisho wa kiongozi huyo kushiriki katika uasi na kunaweza kupuunguzia nguvu utetezi unaotolewa na Dk Kitila kwamba hakuwa sehemu mpango wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani. Zitto, Dk Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba wanasubiri kukabidhiwa barua za kuvuliwa kwao madaraka na katika siku 14 wanapaswa wawe wamewasilisha utetezi wao wakieleza kwa nini wasifukuzwe uanachama kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Dk Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema jana kuwa ilikuwa lazima viongozi hao wavuliwe madaraka hasa baada ya Dk Kitila kukiri kuhusika na waraka ambao anasema ulilenga kushinda kupitia uchaguzi halali ndani ya chama hicho.
“Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?” alihoji Dk Slaa.
 
Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: “Wao nani kawaambia waende kwa waandishi wa habari?”
“Mimi ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?” alihoji Dk Slaa.
Mkutano leo
Mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu  baadhi ya hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu.
Habari zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni “Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu”, badala ya kujibu hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu.
Jana, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa tuhuma za kusema na za kuacha... “Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya hivyo?”
Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: “Kamati Kuu ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu kama chama.”
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda uongozi wa Chadema ukaweka wazi “makosa mengine” ambayo Zitto anadaiwa kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi ya miezi sita. “Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati Kuu imechoka,” alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu.
Habari zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi ndiyo inapaswa kuiandaa.
Wasomi wanena
Akizungumzia mgogoro huo, mtaalamu wa mambo ya siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hali inayoendelea ndani ya Chadema ni matokeo ya vyama vya siasa kutofanya kazi kama taasisi.
“Misingi ya vyama haiweki wazi misingi ya watu kuwa viongozi. Kwa mfano, kesho nikitaka kujiunga na Chadema nitaweza kuwa Mwenyekiti? Misingi ya wazi hakuna,” alisema Mbunda.

Alisema hali ilivyo ndani ya Chadema kwa sasa ni furaha ndani ya CCM, kwani watu wanaona kuwa chama kilichoonekana kuwa mbadala hakiwezi hata kushughulikia mambo yake ya ndani.
Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema vyama vya siasa ni watu au kikundi cha watu wenye malengo na mitazamo tofauti.
“Ukisoma huo waraka utaona kuwa unazungumzia uongozi, upungufu uliopo kwenye uongozi na namna ya kubadili uongozi, mimi binafsi niseme ieleweke kwamba hata kwenye jumuiya yoyote mambo haya yapo hasa kwa kuwa walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi,” alisema. Alisema haoni kwa nini Zitto na Dk Kitila waonekane wahaini kwa kupanga mikakati yao ambayo walitaka kuitekeleza kupitia uchaguzi.
“Mabadiliko ni jambo la kawaida, hali hii ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao inawezekana ikawagharimu Chadema na inaweza kuwagharimu zaidi wakiwafukuza uanachama,” alisema Makulilo.

SOURCE: Mwananchi.

Skendo: Vigogo wa Polisi wadaiwa kumtorosha KAPUYA baada ya Denti aliyedaiwa Kubakwa kumfungulia Kesi...!!

SIKU chache baada ya Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kudaiwa kutoweka nchini kukwepa mkono wa sheria dhidi ya tuhuma za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, vigogo wa polisi wanadaiwa kuhusika kumsaidia kutimkia nje, Tanzania Daima limedokezwa. 

Habari ambazo gazeti hili limezipata, zinaeleza kuwa siku mbunge huyo akikamilisha taratibu za kusafiri, ndiyo siku ambayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilikuwa limekamilisha kufungua jalada la tuhuma zake na liliweka mtego wa kumnasa.

Wakati Polisi Kinondoni wakiweka mtego wa kumnasa, baadhi ya polisi walimjulisha na hata kumsaidia kuhakikisha anasafiri nje ya nchi,” alisema mmoja wa maofisa wa juu wa polisi nchini.

Hata hivyo, kuna utata na kauli zinazopingana kuhusu mbunge huyo. Taarifa nyingine zinasema kuwa mbunge huyo ambaye amepata kuwa waziri, anadaiwa kusafiri kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.

Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini humo miezi miwili hadi mitatu.

Hata hivyo, haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kutuliza upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.

Tayari Profesa Kapuya alishafunguliwa jalada nambaOB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa linamsaka mbunge huyo ndani na nje ya nchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa juzi kuwa watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.

Alisema mtandao wa polisi ni mkubwa, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.

Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana, na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.
Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya, huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.

Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.

Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Gazeti hili limekuwa likiandika namba ya simu ya Prof. Kapuya ambayo huwa anaitumia kutuma ujumbe wa vitisho kwa binti huyo, ingawa kuna vyombo vingine vya habari viliamua kuandika kwa mtazamo tofauti na kumtuhumu dada wa binti aliyebakwa kuwa ni mtu mzima na kuwa ana uhusiano na Kapuya, na wana watoto.

Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda kwa binti huyo.

Tangu gazeti hili lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.

Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilizoanza wiki iliyopita ziliendelea hadi juzi ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

------Tanzania Daima
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI 

Mama Zitto Kabwe amekua akiomba Zitto afukuzwe CHADEMA? soma zaidi hapa

Gazeti la Mwananchi leo November 24 2013 limeandika >>> Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.


“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake, nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”

Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata).

Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo juzi walivuliwa uongozi kutokana na uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili, kuanzia Novemba 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa  kukisaliti chama.

Mbali ya kuwavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo pamoja na  aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama.

Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Katika ufafanuzi wake wa jana, Shida aliwataka wanachama wa Chadema kuwa watulivu kwa maelezo kuwa Zitto hajafukuzwa uanachama, “Siku nyingi walikuwa wanamwinda na hata hilo jambo ambalo Chadema wanasema amefanya, hawana uhakika nalo.”
Juzi wakati akisoma uamuzi wa Kamati Kuu,  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema wamebaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
Alisema kikundi hicho vinara wake wapo wanne,  Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne ambaye alieleza kuwa hajatambulika na anatumia jina la M2.

Stori imetoka mwananchi.co.tz


Use Facebook to Comment on this Post

SOURCE: Millardayo.com