Katika
kazi yoyote ile inayohusu maisha ya mwanadamu moja kwa moja kama vile
Udaktari, Uuguzi, Ufamasia n.k., wasomi huwa hawaruhusiwi kufanya kazi
katika maeneo hayo nyeti kabla ya kula kiapo baada ya kozi za masomo
yao.
Madaktari kwa mfano, wana kiapo chao ambacho sehemu yao huapa kwa kusema, "I will respect the privacy of my patients, for their problems are not disclosed to me that the world may know." Yaani, anaapa kuwa ataheshimu na kulinda siri za mgonjwa kwani hapewi maelezo hayo ili aujulishe ulimwengu.
Lakini inaelekea katika kila hali, mwanadamu ni rahisi kusahau ama kudharau kiapo alichokula na kwenda kinyume na inavyokusudiwa kama ambavyo imetokea kwa daktari mmoja huko Ghana aliyewabaka wateja aliokuwa ameahidi kuwatoa mimba, ama daktari wa Urusi aliyempiga ngumi kifuani mgonjwa wa tatizo la moyo na kumsababishia mauti, au huyu wa Marekani, Dk Nikita Levy aliyekuwa akiwarekodi wateja wake wakati akiwahudumia kama mtaalamu wa masuala ya uzazi ya wanawake.
Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali alikokuwa akifanyia kazi daktari huyu amekuwa msaada baada ya kuripoti kwa uongozi wa hospitali hiyo kuwa anahisi Dk Nikita anarekodi wagonjwa kwa kutumia kalamu yake maalumu.
Kisichofahamika ni alikokuwa akipeleka au namna alivyokuwa akizitumia video na picha hizo. Pengine kwa manufaa yake

Zaidi ya wanawake 3,800 kati ya zaidi ya 9,000 waliohudhuria katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital iliyopo Baltimore na kuonwa na Dk Nikita, sasa wameruhusiwa na hakimu kujiunga katika kesi ya madai dhidi ya hospitali iliyomwajiri Dk Nikita, aliye marehemu kwa sasa; Alijitoa uhai baada ya kutambua alikuwa anachunguzwa kwa tuhuma hizo pale alipozuiwa kuonana na wagonjwa baada ya kuhojiwa na maafisa usalama wa Hopkins Februari 5, 2013 kutokana na taarifa zilizoripotiwa na mfanyakazi mmoja aliyehisi kuwa kifaa kinachofanana na kalamu alichokuwa anakivaa Dk Nikita kwenye ukosi kilikuwa na kamera yenye uwezo wa kurekodi na alikuwa akiitumia kinyume na sheria na taratibu.
Polisi wa Hopkins walitoa taarifa kwa maofisa wa Jiji la Baltimore siku iliyofuata, ambao mara moja walipekua nyumbani kwa Dk Nikita na kufanikiwa kupata vidhibiti na ushahidi ikiwa ni pamoja na seva za kielektroniki alizokuwa akizitumia.
Madai ya fidia yaliyofikishwa mahakamani na mawakili wa wanawake hao ni ya kupigwa picha na kurekodiwa bila kufahamishwa, bila kuombwa ridhaa, bila ya kufahamishwa na na kwa wafanyakazi na uongozi mzima wa hospitali hiyo kuwa wazembe kiasi cha kutokutambua, kuzuia na kuripoti vitendo hivyo.
Mawakili wa hospitali hiyo wameonesha ushirikiano na mawakili wa upande wa madai na hiyo imewapa matumaini kuwa wanaweza kumaliza kadhia hii.
Uongozi wa Johns Hopkins umetoka tamko Ijumaa ya leo, Novemba 1, 2013 kwa matarajio yakufikia suluhisho mapema.
Source: wavuti.com
No comments:
Post a Comment