Jitihada za kumdhamini mbunge wa Jimbo la Ukerewe (CHADEMA) Ndugu Salvatory Machemli zimeshindikana ikiwa ni siku ya saba tangu awekwe mahabusu baada ya kufutiwa dhamana na Maahakama ya Wilaya ya Ukerewe.
Kaimu Hakimu wa mahakama ya
wilaya ya Ukerewe, Mrisho Abed alisema kuwa amri hiyo ya
kwenda rumande kwa siku 14 ilitolewa baada ya
mshitakiwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Alisema sheria
ya makosa ya jinai namba 20 iliyofanyiwa malekebisho mwaka 2002
kifungu cha 148 katika vifungu vidogo vya (5),(3)(C) mahakama inapewa
mamlaka ya kufuta dhamana ya mshitakiwa.
Hakimu Abed alisema chombo pekee chenye mamlaka ya kuitengua amri hiyo ni Mahakama Kuu.
Alikazia kuwasi hiyo ingekuwa chini yake, asingetoa dhamana tena kwa mshitakiwa hadi isikilizwe na kumalizika.
No comments:
Post a Comment