MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi Wilaya
ya Ukerewe Faustine Kashyeni, imemuamuru Mbunge wa Jimbo la Ukerewe
Salvatory Machemli pamoja na wadhamini wake watatu kwenda rumande siku
14 baada ya kuidharau mahakama kufuatia kesi ya utapeli na madai
inayomkabiri.
Inatajwa kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita mbunge huyo
alikopa fedha kutoka kwa marafiki zake kwa ahadi ya kuzirejesha, ili
kunua nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 130 ambapo alifanikiwa
kulipa kiasi cha shilingi milioni 50 na akawa anadaiwa milioni 130
ambazo alipaswa kulipa kwa wakati lakini mbunge huyo hakufanya hivyo
kiasi cha kuwa mtu wa kula chenga na ahadi za kesho kesho zisizotimia.
Kuona hivyo marafiki waliomkopesha fedha waliamua kulifikisha mahakamani
suala hilo kwa kufungua kesi ya madai ambapo mdaiwa alikiri kuchukuwa
fedha zilizotajwa.
Mara kadhaa Machemli alitakiwa kuhudhuria mahakamani lakini hakufanya
hivyo hali iliyoipelekea chombo hicho ambacho ni moja kati ya mihimili
ya dola kuchukuwa uamuzi wa kuwasweka rumande wadhamini wake wote watatu
ambao walipaswa kumwakilisha mahakamani na hawakufanya hivyo, kisha hii
leo mbunge huyo naye akakamatwa na kuwekwa ndani ili iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
Watatu wengine walio kumbana na adhabu hiyo ni pamoja na Shelfu
Ngelezya, Max Mhogo na Consolata Machemli ambao walikamatwa awali na
tayari wameshamaliza adhabu zao.
SOURCE:GSENGO
No comments:
Post a Comment