Paris, Ufaransa. Vita
ya kusaka timu nne za Ulaya za mwisho kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014
inaanza leo kwa Ufaransa na Ureno kupigania heshima ya kuugana na vigogo
wenzao Hispania na Ujerumani waliotangulia Brazil.
Ureno inayoongozwa na Cristiano Ronaldo watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Sweden, ambayo itakuwa nchini ya Zlatan Ibrahimovic.
Mabingwa wa zamani Ufaransa wenyewe watakuwa
ugenini Kiev kuivaa Ukraine wana matumaini kidogo ya kufuzu, lakini si
kwa utata kama ule wa 2010 wakati waliposubiri hadi bao la mkono la
Thierry Henry liliitoa Ireland.
Mechi nyingine itawakutanisha Ugiriki dhidi ya
Romania, huku timu ndogo ya Iceland itakuwa ikisaka nafasi ya kuwa taifa
dogo kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali hizo wakati
watakapoikabili Croatia.
Kocha wa Ureno, Paulo Bento, ambayo aliiongoza
timu hiyo kufuzu kwenye nusu fainali ya Euro mwaka jana anajua kuwa ana
mategemeo mamakubwa.
“Najua kwa nini nina matarajio makubwa kwa sababu
ni Kombe la Dunia ndani ya Brazil, japokuwa lengo letu hilo litabaki
hivyo hata kama tutakwama,” aliimbia Fifa.com.
“Mechi dhidi ya Sweden itakuwa ni ngumu:
Tunajiamini na tunawaheshimu wapinzani wetu, kuliko kitu chochote. Hata
hivyo tunajiamini kwamba tukwenda Brazil 2014.”
Watu wengi wanasikitika kuwa moja kati ya Ronaldo
au Ibrahimovic ataikosa Brazil, lakini mshambuliaji wa PSG amesema timu
yake inastahili kucheza Kombe la Dunia na watakuwepo katika upangwaji wa
ratiba Desemba 6 mjini Mata de Sao Joao.
“Tuna mechi ngumu, lakini hiyo ni hali nzuri kwetu,” alisema Ibrahimoivic.
“Nimeona wachezaji wawili tofauti, wakiwa kwenye
kiwango cha juu wakiwakilisha nchi zao katika hatua muhimu,” alisema
Ibrahimovic.
“Kwanza haitakiwa kuifanya mechi hiyo kwa wawili
hao tu, hii ni mechi kati ya Sweden dhidi ya Ureno nafikiri ikizungumza
hivyo ni vizuri zaidi.”
Ukraine itawakaribisha Ufaransa walio katika hatari ya kukosa
Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1994 pia hawataki kurudia makosa
ya 2010 yaliyotokea ndani na nje ya uwanja kilichofanya wachezaji
kugomea mazoezi.
Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps ambaye 1998,
alikuwa nahodha wa kwanza wa Ufaransa kunyanyua Kombe la Dunia wakati
walipoifunga Brazil jijini Paris, amesema wachezaji wake wanachukulia
kwa umakini mkubwa mchezo huo dhidi ya Ukraine.
“Wachezaji wanakuwa uwanjani, lakini ni kocha ndiye anayeongoza miguu yao,” alisema nyota huyo wa zamani Juventus.
No comments:
Post a Comment