Thursday, 28 November 2013

KOMBE LA DUNIA KUTUA MWANZA KWA MARA YA KWANZA, KUWEKA HISTORIA.

Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia litapokelewa Mkoani Mwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, mbele ya waandishi wa habari na kamati ya maandalizi ya ujio huo katika ukumbi wa Mwanza Hotel hivi leo.
 
Ndikilo amesema hii ni mara ya kwanza kwa kombe hilo kupokelewa katika Mkoa huo na akawataka wanachi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kulipokea,amesema na kuongeza kuwa "Mhe shimiwa Rais ambaye yupo ziarani katika Mkoa wa Simiyu amekubali kulilaki kombe hilo katika mkoa wetu wa Mwanza hii ni heshima kubwa kama wananchi wa Mkoa huu na wapenda michezo kwa ujumla.
 
Amesema kombe hilo litawasili katika uwanja wa ndege wa mwanza majira ya saa tatu asubuhi na badae kupelekwa katika uwanja wa CCM Kirumba, ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya wananchi watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Coca Cola Nchini bw. Eyebolt Gretchen, amesema ujio wa Kombe hilo kwa mara ya tatu katika nchi ya Tanzania nia pamoja na amani ya nchi iliyopo na ukarimu wa watu wake, Miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimekuwa na utulivu hata kufanya kutembelewa na kombe la Dunia ni Tanzania, amesema na kuongeza kwamba, kama Coca cola wamekuwa mstari wa mbele kwenye jitihada za kukuza soka nchini ikiwapo mashindano ya Kopa Coca cola.
 
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu amewahakikishia wanachi wote wa Mkoa wa Mwanza amani na utulivu, aidha amewaomba wananchi kutokuja wanjani hapo wakiwa na watoto wadogo ili kuepusha adha wanayoweza kupata watoto hao" Labda niombe ndugu zangu kwa wale watoto wadogo ni vema wakaachwa nyumbani kuepuka usumbufu". alisema na kuongeza kuwa watu hawataruhusiwa kusogea karibu na eneo la Pitch ya uwanja huo.
 
Hii ni mara ya tatu kombe hilo linakuja hapa nchini ambapo mara zote limekuwa likipokelewa na kulakiwa na wananchi waishio katika Mkoa wa Dar es Salaam. 
 
Wadadisi wa mambo wanasema kwamba, ujio wa kombe hilo si tu kwamba linakuja kutazamwa na wanachi wa Mwanza bali pia ni frsa nzuri kwa mkoa huo kujitangaza kimataifa lakini pia kutangaza rasilimali zinazo patikana katika Mkoa huo alkini pia iwe chachu kwa vingozi kuona kuna umuhimu wa kuipa kipaumbele michezo yote, anasema Mashaka Baltazari mwandishi mwandamizi wa Jambo Leo na Mwakilishi Mkoani Mwanza.

SOURCE: AFISA HABARI MKOA
                  MWANZA.
 

Tuesday, 26 November 2013

Wananchi ‘wawashtaki’ viongozi kwa mbunge

Wasema hawachukui hatua za kushughulikia kero zinazowakabili kwa muda mrefu
Wananchi  wa Mtaa wa Mwanzomgumu katika Kata ya Bigwa,  Manispaa ya Morogoro, wamewashtaki kwa mbunge wa jimbo hilo, Abdullaziz Abood, viongozi wa serikali ya mtaa huo, kwa kile walichokielezea kuwa ni kushindwa kuwatumikia.
Wananchi hao walisema tatizo hilo pia liko katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ambayo haifanyi jitihada za kutosha, ili kuwaondolea kero mbalimbali zikiwemo kukosa baadhi ya huduma muhimu.
Abood alipita katika mtaa huo akiwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa Kata za Bigwa, Mindu na Mkundi ambapo pia alikabidhi  vifaa mbalimbali.
 Msaada wa vifaa hivyo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake za wakati wa kampeni  za uchaguzi wa mwaka 2010, ni pamoja na  vyerehani, mabomba ya kusambazia maji, mawe, kokoto, mifuko ya saruji, mchanga na hundi za fedha.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, wananchi wa Mtaa Mwanzomgumu, walisimamisha msafara wa mbunge Abood na  kumlalamikia kitendo cha viongozi wao kutowajali kwa maana ya kushughulikia kero zao.
Wananchi hao walisema eneo lao linakabiliwa na matatizo mengi, lakini viongozi wao hawafanyi jitihada za kupunguza kama si kumaliza kabisa matatizo hayo.
Walisema matatizo hayo ni pamoja na ubovu wa barabara, kutozwa Sh100 kwa kila ndoo ya maji, ili kuchangia huduma hiyo na kukosekana kwa kituo cha polisi.
Baada ya malalamiko hayo, Abood aliwaita viongozi wa eneo hilo ili wajadiliane naye kuhusu namna ya kutatua matatizo hayo, lakini waligoma.
Badala yake, walimtaka aende walikokuwa, lakini naye alikataa kwa sababu ratiba ya ziara yake ilimbana.

SOURCE: MWANANCHI.

Diwani amkosoa Lissu

Mwanasheria mkuu wa Chadema,Tundu Lissu. 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Novemba25  2013  saa 11:36 AM
 
Dar es Salaam. Wakili wa kujitegemea na Diwani wa Kata ya Mabogini mkoani Kilimanjaro (Chadema), Albert Msando ameeleza kasoro nne za kisheria ambazo zimefanywa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu wakati wa kutoa hukumu kwa makosa yaliyofanywa na makada wa chama hicho, Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msando alisema Katiba ya Chadema inaeleza kuwa kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi.
“Tunaomba Lissu aeleze kwa njia ileile aliyotumia kueleza umma wa Watanzania uamuzi wa Kamati Kuu, siku na tarehe ambayo Dk Kitila na Zitto walipewa mashtaka yao kwa maandishi na atoe nakala ya majibu yao kwa maandishi kama yapo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema,” alisema na kuongeza:
“Aeleze ni utaratibu gani ulitumika kuwajadili kwenye kikao cha Kamati Kuu, kufikia uamuzi na kuwapa adhabu ya kuwavua madaraka wakati hawajapewa mashtaka hayo kwa maandishi kama Katiba inavyosema, kisha Kamati Kuu kwenda kwenye vyombo vya habari na kueleza kuhusu uamuzi huo na kutoa siku 14 ili wajieleze.”
Alisema Lissu hatakiwi kutoa majibu ya jumla, bali kueleza utaratibu, sheria na utawala bora gani uliotumika kuchukua uamuzi huo dhidi ya Zitto na Dk Kitila. Alisema Lissu pia anatakiwa kueleza aina ya ushahidi alionao ambao ulitumika kuwahukumu.

SOURCE. MWANANCHI.

Monday, 25 November 2013

Rage ampinga Malinzi kweupe

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) katiba ya Simba katika mkutano alioufanya jana Jumapili kuhusu kusimamishwa kwake. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo, Barabara ya Msimbazi, Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga. 
Na Sosthenes Nyoni, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Novemba25  2013  saa 14:27 PM
 
Kwa ufupi
 
Awali, Rais wa TFF, Jamal Malinzi akizungumza na Wanahabari alimtaka Rage aitishe mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba ndani ya siku 14 kuanzia Novemba 23. 

Rage amemteua Wambura  kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba.
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage amepinga agizo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linalomtaka aitishe mkutano wa mabadiliko ya katiba ndani ya siku 14 na kusema endapo msimamo huo utasisitizwa basi atajiuzulu.
Awali, Rais wa TFF, Jamal Malinzi akizungumza na Wanahabari alimtaka Rage aitishe mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba ndani ya siku 14 kuanzia Novemba 23.
“Kutokana na Mgogoro uliopo Simba hivi sasa, kamati ya utendaji ya TFF inamwagiza mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kuitisha mkutano mkuu wa dharura ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
“Uamuzi huu umefanywa kwa kuzingatia ibara ya 1(6) ya katiba ya Simba inayosema Simba Sports Klabu ni mwanachama wa TFF, itaheshimu katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF,” alisema Malinzi.
Lakini jana mwenyekiti wa Simba, Rage akizungumzia agizo hilo la TFF alisema hawezi kuitisha mkutano huo kwa shinikizo la shirikisho hilo.
“Katiba ya TFF ibara 31(1-5) inasema mjumbe wa kamati ya utendaji atakosa sifa kama atakosa mambo manne, ataandika barua kujiuzulu, haudhurii mikutano minne iliyoitishwa na mwenyekiti  halali, kama atakuwa mgonjwa amelala kitandani miezi 12  mgonjwa na amekutwa na kosa la jinai,” alisema Rage.
Alisema,” nimesikitishwa na agizo la TFF kunitaka niitishe  mkutano ndani ya siku 14, wamenukuu ibara ya 1(6), Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, nitaheshimu katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF, hatuwezi kuheshimu kuvunja katiba ya TFF, mimi naambiwa nivunje katiba ya TFF naambiwa nivunje katiba ya Simba.”
“Tena wamekwenda mbali wananitaka niitishe mkutano ndani ya siku 14 sijui wameitoa wapi, haipo kwenye katiba ya TFF wala Simba, mimi msimamo wangu kama mwenyekiti wa Simba siitishi mkutano nalindwa na katiba,” alisema Rage.
Akizungumzia kamati ya utendaji iliyoketi na kumsimamisha, Rage alisema ilikuwa batili kutokana na kuongozwa na mtu ambaye hatambuliki katika katiba ya klabu yake ya Simba.
“Kamati ya utendaji ya Simba inakamilika kwa kuwa na mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe saba waliochaguliwa katika uchaguzi halali, hakuna  sehemu inayomtaja kaimu mwenyekiti au umewahi kuona wapi mtu ana kaimu na kukaimu, huyo Itangire si amewekwa tu pale, alichaguliwa na nani?” Alihoji Rage. Alijitapa kwa kusema hatua yake ya kwenda kuzunguza makao makuu ya klabu yake imedhihirisha yeye ndiye mwanaume wa kweli na aliwaponda wapinzani wake kwamba ni waoga kutokana na kumjadili mafichoni.
“Siku zote ukitaka kupindua nchi unaanza kuteka Ikulu, mimi ndiyo mwanaume wa kweli siyo hao wanaoongelea huko uchochoroni huo si uoga?” alijigamba Rage. 
 
 Katika hatua nyingine, Rage amemteua Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba na kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Rahma Al Kharoosi aliyejizulu kutokana na kutingwa na majukumu.
 
SOURSE: MWANANCHI. 

Zitto ajiweka njia panda

“Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?”  Dk Slaa. 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Jumanne,Novemba26  2013  saa 8:40 AM
 
Kwa ufupi

Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.
 
Dar es Salaam. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amejiweka katika mazingira magumu zaidi kisiasa ndani ya chama hicho, kutokana na shaka kubwa iliyougubika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam juzi.
Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.
Leo, uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
Miongoni mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa nyadhifa zao.
Mchange na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM wanakoendeleza harakati zao za kisiasa.
Jana, Machange alipotafutwa, alisema: “Mimi sikuwahi kuondoka Chadema, nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema nimeondoka.
Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu.
“Mimi ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote, walioondoka ni Mwampamba na Shonza.” Mwampamba alisema: “Nilijitokeza pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu.”
Kuwepo kwao katika mkutano wa Zitto kunaweza kutumiwa na uongozi wa Chadema kuwa uthibitisho wa kiongozi huyo kushiriki katika uasi na kunaweza kupuunguzia nguvu utetezi unaotolewa na Dk Kitila kwamba hakuwa sehemu mpango wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani. Zitto, Dk Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba wanasubiri kukabidhiwa barua za kuvuliwa kwao madaraka na katika siku 14 wanapaswa wawe wamewasilisha utetezi wao wakieleza kwa nini wasifukuzwe uanachama kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Dk Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema jana kuwa ilikuwa lazima viongozi hao wavuliwe madaraka hasa baada ya Dk Kitila kukiri kuhusika na waraka ambao anasema ulilenga kushinda kupitia uchaguzi halali ndani ya chama hicho.
“Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?” alihoji Dk Slaa.
 
Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: “Wao nani kawaambia waende kwa waandishi wa habari?”
“Mimi ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?” alihoji Dk Slaa.
Mkutano leo
Mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu  baadhi ya hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu.
Habari zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni “Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu”, badala ya kujibu hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu.
Jana, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa tuhuma za kusema na za kuacha... “Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya hivyo?”
Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: “Kamati Kuu ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu kama chama.”
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda uongozi wa Chadema ukaweka wazi “makosa mengine” ambayo Zitto anadaiwa kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi ya miezi sita. “Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati Kuu imechoka,” alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu.
Habari zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi ndiyo inapaswa kuiandaa.
Wasomi wanena
Akizungumzia mgogoro huo, mtaalamu wa mambo ya siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hali inayoendelea ndani ya Chadema ni matokeo ya vyama vya siasa kutofanya kazi kama taasisi.
“Misingi ya vyama haiweki wazi misingi ya watu kuwa viongozi. Kwa mfano, kesho nikitaka kujiunga na Chadema nitaweza kuwa Mwenyekiti? Misingi ya wazi hakuna,” alisema Mbunda.

Alisema hali ilivyo ndani ya Chadema kwa sasa ni furaha ndani ya CCM, kwani watu wanaona kuwa chama kilichoonekana kuwa mbadala hakiwezi hata kushughulikia mambo yake ya ndani.
Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema vyama vya siasa ni watu au kikundi cha watu wenye malengo na mitazamo tofauti.
“Ukisoma huo waraka utaona kuwa unazungumzia uongozi, upungufu uliopo kwenye uongozi na namna ya kubadili uongozi, mimi binafsi niseme ieleweke kwamba hata kwenye jumuiya yoyote mambo haya yapo hasa kwa kuwa walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi,” alisema. Alisema haoni kwa nini Zitto na Dk Kitila waonekane wahaini kwa kupanga mikakati yao ambayo walitaka kuitekeleza kupitia uchaguzi.
“Mabadiliko ni jambo la kawaida, hali hii ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao inawezekana ikawagharimu Chadema na inaweza kuwagharimu zaidi wakiwafukuza uanachama,” alisema Makulilo.

SOURCE: Mwananchi.

Skendo: Vigogo wa Polisi wadaiwa kumtorosha KAPUYA baada ya Denti aliyedaiwa Kubakwa kumfungulia Kesi...!!

SIKU chache baada ya Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kudaiwa kutoweka nchini kukwepa mkono wa sheria dhidi ya tuhuma za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, vigogo wa polisi wanadaiwa kuhusika kumsaidia kutimkia nje, Tanzania Daima limedokezwa. 

Habari ambazo gazeti hili limezipata, zinaeleza kuwa siku mbunge huyo akikamilisha taratibu za kusafiri, ndiyo siku ambayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilikuwa limekamilisha kufungua jalada la tuhuma zake na liliweka mtego wa kumnasa.

Wakati Polisi Kinondoni wakiweka mtego wa kumnasa, baadhi ya polisi walimjulisha na hata kumsaidia kuhakikisha anasafiri nje ya nchi,” alisema mmoja wa maofisa wa juu wa polisi nchini.

Hata hivyo, kuna utata na kauli zinazopingana kuhusu mbunge huyo. Taarifa nyingine zinasema kuwa mbunge huyo ambaye amepata kuwa waziri, anadaiwa kusafiri kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.

Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini humo miezi miwili hadi mitatu.

Hata hivyo, haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kutuliza upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.

Tayari Profesa Kapuya alishafunguliwa jalada nambaOB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa linamsaka mbunge huyo ndani na nje ya nchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa juzi kuwa watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.

Alisema mtandao wa polisi ni mkubwa, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.

Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana, na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.
Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya, huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.

Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.

Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Gazeti hili limekuwa likiandika namba ya simu ya Prof. Kapuya ambayo huwa anaitumia kutuma ujumbe wa vitisho kwa binti huyo, ingawa kuna vyombo vingine vya habari viliamua kuandika kwa mtazamo tofauti na kumtuhumu dada wa binti aliyebakwa kuwa ni mtu mzima na kuwa ana uhusiano na Kapuya, na wana watoto.

Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda kwa binti huyo.

Tangu gazeti hili lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.

Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilizoanza wiki iliyopita ziliendelea hadi juzi ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

------Tanzania Daima
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI 

Mama Zitto Kabwe amekua akiomba Zitto afukuzwe CHADEMA? soma zaidi hapa

Gazeti la Mwananchi leo November 24 2013 limeandika >>> Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.


“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake, nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”

Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata).

Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo juzi walivuliwa uongozi kutokana na uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili, kuanzia Novemba 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa  kukisaliti chama.

Mbali ya kuwavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo pamoja na  aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama.

Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Katika ufafanuzi wake wa jana, Shida aliwataka wanachama wa Chadema kuwa watulivu kwa maelezo kuwa Zitto hajafukuzwa uanachama, “Siku nyingi walikuwa wanamwinda na hata hilo jambo ambalo Chadema wanasema amefanya, hawana uhakika nalo.”
Juzi wakati akisoma uamuzi wa Kamati Kuu,  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema wamebaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
Alisema kikundi hicho vinara wake wapo wanne,  Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne ambaye alieleza kuwa hajatambulika na anatumia jina la M2.

Stori imetoka mwananchi.co.tz


Use Facebook to Comment on this Post

SOURCE: Millardayo.com

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWA WANANCHI YA OKTOBA 2013


           

HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI FEBRUARI 2013


              

Dakika 6 za kauli ya Zitto Kabwe ya msimamo baada ya kuvuliwa vyeo Chadema. @ZittoKabwe


Zitto Kabwe alizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa habari kuhusu ishu yake ya kuvuliwa vyeo Chadema baada ya kamati kukaa, bonyeza play hapo chini utazame alichosema ndani ya dakika 6.
           

Use facebook to comment on this post

SOURCE: Millardayo.com

Barack Obama amem-follow kwenye twitter mwimbaji huyu Mtanzania.

Hii itakuwa ni kwa mara kwanza kwa mwimbaji wa Tanzania na pengine Afrika kuwa followed na Rais Barack Obama wa Marekani kwenye twitter ambae ana zaidi ya followers milioni 40 lakini yeye anafollow watu laki sita.
Vanessa Mdee ameingia kwenye list ya watu laki sita ambao Rais Barrack Obama ana wa-follow sasa hivi ambapo baada ya Rais huyu kufollow, kwa furaha Vanessa alishare kwenye instagram screenshot ya ukurasa wake wa twitter ukionyesha Barack Obama ameanza kum-follow.
Kama ilivyo twitter, hii inamaanisha ana Vanessa ana uwezo wa kumuandikia msg binafsi kwenye inbox Rais Obama.

SHABIKI MAARUFU STIVEN WA YANGA AINGIA RASMI BONGO MOVIE


           

MCHINA AJITOSA LIVE KUIGIZA BONGO MOVIE 2013


          

VIDIO MPYAA YA SNURA "NIMEVURUGWA" YATISHA.


           

Mwili wa mwanamamke wakutwa kichakani ukiwa umekatwa kichwa na kufungwa kamba.






Kwenye kijiji cha Nyamira wanakijiji wameamka na kukuta mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa kichwa na kutelekezwa pamoja na kufungwa mikono kwa kamba.


Mwili huo  ambao unaonyesha kuwa ni mwanamke mwenye miaka kati ya 25 hadi 35 amekutwa umevaa  jeans pamoja blouse nyeusi na kutupwa pembeni ya kijito cha maji mida ya saa 12 na nusu asubuhi.


Wanakijiji walishtuka na tukio hilo na kusema kwamba ni kitu cha ajabu kwenye kijiji chao na polisi wa Kenya wametangaza familia yoyote itakayoona kuna mtu amepotea nyumbani kwao atoe taarifa.


Hii ni video ya  ripoti kamili ya NTV ya Kenya



SOURCE: Millardayo.com 

Use facebook to comment this video.

VIDEO YA CHADEMA KUHUSU KUMVUA MADARAKA YOTE MH:ZITTO KABWE NA WENZAKE WAWILI



Friday, 15 November 2013

Timu 11, zitakazofuzu kwa Kombe la Dunia zitaanza kupambana baada ya wiki wakati wa michezo ya mtoano wenye timu 32.


Paris, Ufaransa. Vita ya kusaka timu nne za Ulaya za mwisho kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014 inaanza leo kwa Ufaransa na Ureno kupigania heshima ya kuugana na vigogo wenzao Hispania na Ujerumani waliotangulia Brazil.
Ureno inayoongozwa na Cristiano Ronaldo watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Sweden, ambayo itakuwa nchini ya Zlatan Ibrahimovic.
Mabingwa wa zamani Ufaransa wenyewe watakuwa ugenini Kiev kuivaa Ukraine wana matumaini kidogo ya kufuzu, lakini si kwa utata kama ule wa 2010 wakati waliposubiri hadi bao la mkono la Thierry Henry liliitoa Ireland.
Mechi nyingine itawakutanisha Ugiriki dhidi ya Romania, huku timu ndogo ya Iceland itakuwa ikisaka nafasi ya kuwa taifa dogo kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali hizo wakati watakapoikabili Croatia.
Kocha wa Ureno, Paulo Bento, ambayo aliiongoza timu hiyo kufuzu kwenye nusu fainali ya Euro mwaka jana anajua kuwa ana mategemeo mamakubwa.
“Najua kwa nini nina matarajio makubwa kwa sababu ni Kombe la Dunia ndani ya Brazil, japokuwa lengo letu hilo litabaki hivyo hata kama tutakwama,” aliimbia Fifa.com.
“Mechi dhidi ya Sweden itakuwa ni ngumu: Tunajiamini na tunawaheshimu wapinzani wetu, kuliko kitu chochote. Hata hivyo tunajiamini kwamba tukwenda Brazil 2014.”
Watu wengi wanasikitika kuwa moja kati ya Ronaldo au Ibrahimovic ataikosa Brazil, lakini mshambuliaji wa PSG amesema timu yake inastahili kucheza Kombe la Dunia na watakuwepo katika upangwaji wa ratiba Desemba 6 mjini Mata de Sao Joao.
“Tuna mechi ngumu, lakini hiyo ni hali nzuri kwetu,” alisema Ibrahimoivic.
“Nimeona wachezaji wawili tofauti, wakiwa kwenye kiwango cha juu wakiwakilisha nchi zao katika hatua muhimu,” alisema Ibrahimovic.
“Kwanza haitakiwa kuifanya mechi hiyo kwa wawili hao tu, hii ni mechi kati ya Sweden dhidi ya Ureno nafikiri ikizungumza hivyo ni vizuri zaidi.”

Ukraine itawakaribisha Ufaransa walio katika hatari ya kukosa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1994 pia hawataki kurudia makosa ya 2010 yaliyotokea ndani na nje ya uwanja kilichofanya wachezaji kugomea mazoezi.
Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps ambaye 1998, alikuwa nahodha wa kwanza wa Ufaransa kunyanyua Kombe la Dunia wakati walipoifunga Brazil jijini Paris, amesema wachezaji wake wanachukulia kwa umakini mkubwa mchezo huo dhidi ya Ukraine.
“Wachezaji wanakuwa uwanjani, lakini ni kocha ndiye anayeongoza miguu yao,” alisema nyota huyo wa zamani Juventus.

Ajira ngumu tishio jipya kwa ustawi wa watoto

Watoto hawa ni miongoni mwa watoto wengi wanaofanya kazi za kugonga kokoto na kuchonga matofali kisiwani Pemba.  Watoto wengi wanatumikishwa katika ajira hiyo ngumu, huku wakikosa haki yao ya kupata elimu. Picha na Talib Ussi. 
 
 
 
Na Talib Ussi, Mwananchi
Posted  Ijumaa,Novemba15  2013  saa 11:47 AM
 
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi kupitia mradi wa kupambana na ajira ngumu kwa watoto,  zaidi ya watoto 15,000 wanajishughulisha na ajira tena zile ngumu.
Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikitimiza miaka 50 tangu Mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyojenga mazingira mazuri ya maendeleo, visiwa vya Unguja na Pemba vimeathirika na ajira ngumu zinazowahusisha watoto.
Hicho ni kikwazo kinachoweza kuifanya Zanzibar ishindwe kuyafikia Malengo ya Milenia, ambayo yanataka hadi kufikia mwaka 2015 watoto wote wapate fursa na haki za msingi za elimu.
Vichocheo vya  ajira kwa watoto
Kwa Zanzibar sababu ni nyingi, ikiwamo wazazi kutokuwa na mwamko wa kuwasomesha watoto wao na kutamalaki kwa umaskini katika familia nyingi.
Hata hivyo,  wapo wazazi walioamua tu kuwatumikisha watoto wao katika ajira ngumu, huku wakisingizia kuwa wanafanya hivyo kwa sababu ya ugumu wa maisha.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi kupitia mradi wa kupambana na ajira ngumu kwa watoto, zaidi ya watoto 15,000 wanajishughulisha na ajira tena zile ngumu.
 Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) ambacho ni sehemu ya washiriki wa mradi, Sheha Haji Dau, anasema waliwatembelea watoto zaidi ya 264 na kubaini 80 wanaishi katika mazingira hatarishi kwa kujishughulisha na ajira ngumu.
Baada ya kuwabaini anasema wamekuwa wakihakikisha wanarudi shule kama anavyosema: “Kijiji cha Charawe pekee watoto 16 wamerudishwa shule. Wanaendelea vizuri na masomo, huku tukitoa elimu kwa wazazi wafuatilie maendeleo yao. ‘’
Hali mbaya Pemba
Kisiwa cha Pemba kinatajwa kuathirika zaidi kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hata ndani ya familia zao.
Mratibu wa asasi ya kiraia inayoshughulikia mapambano ya ajira ngumu za watoto katika Mkoa wa Kaskazini Pemba  (Kukhawa), Mgeni Hamad Othman anasema ajira za watoto zimerudisha nyuma maendeleo ya sekta ya elimu katika kisiwa cha Pemba.
 
‘Mkoa wa Kaskazini ambapo naufanyia kazi, ajira mbaya za watoto zimetawala na kuathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu kwa maendeleo ya Taifa,’’ anasema.
Hata hivyo, anashukuru kuwa kupitia mradi huo wa miaka mitatu, wamefanikiwa kuwarudisha shule watoto 106 wanaosoma katika shule mbalimbali.
Akitoa mfano wa watoto katika maeneo ya Mwambe, vitongoji na Micheweni, anasema watoto wamekuwa wakifanya kazi za kugonga kokoto na uchongaji wa matofali.
Ushuhuda
Mkazi wa Mwamba, Mcha Makame Bahani anawasimamia watoto wapatao saba anaosema, asubuhi wanafanya kazi ya kugonga kokoto ili wapata fedha za matumizi, kisha baadaye wanakwenda shule.
‘Ni kweli ajira za watoto kugonga kokoto zipo Mwamba kwa wingi, lakini sababu kubwa  tunakabiliwa na umaskini  uliokithiri. Hatuna ajira na Serikali haijaweka mikakati ya kutuwezesha miradi midogo midogo,’’ anasema.
Naye mtoto   Mariam Daud Hamad (16), anakiri kuwa kugonga kokoto ndiyo kazi yake ya kila siku kuanzia asubuhi hadi jioni. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa Mariam hakuwahi kupelekwa shule na wazazi.
‘Kwa siku nzima napata madebe 12 ambapo debe moja linauzwa kwa Sh150 mimi sijapelekwa shule lakini nikipelekwa nipo tayari kusoma,’’anaeleza.
Kwa upande wake mchuuzi katika soko la Wesha, lililopo Chakechake,  Kai Kombo Omar anasema iliwachukua miezi sita kuwapiga marufuku wanafunzi wa shule 27 waliokuwa sokoni hapo kuparua samaki.
‘Sisi katika soko la Wesha tumefanikiwa na kukomesha ajira mbaya kwa watoto, kama unavyoona hakuna mtoto hapa anayefanya kazi za kuparua samaki na kuchukuwa mizigo,’’ anaeleza.
Mratibu wa Kukhawa anasema katika utafiti walioufanya katika Shehia moja tu ya Mwambe, watoto 280 wamebainika kufanya kazi ngumu, ambapo asasi yake imo mbioni kuwasaidia na kuwarudisha shule.
‘Ajira za watoto ni changamoto kubwa Pemba kutokana na familia kukabiliwa na hali ngumu ya maisha, sasa sijuwi itakuwaje mradi huu utakapomaliza muda wake,’’anasema.
Ofisa Mwandamizi wa   asasi ya Piro, inayojihusisha na watoto walio kwenye ajira mbaya katika Wilaya ya Micheweni, Sada Hamad Mbarouk anasema wilaya hiyo imeathirika kwa kiasi kikubwa. 
‘Wilaya ya Micheweni Pemba imeathirika na ajira mbaya za watoto, ambapo tayari tumewafikia zaidi ya watoto 562 ambao wamerudi shule,’’ anasema.
Watoto wanaorudishwa shule wamekuwa wakisaidiwa madaftari,viatu pamoja na vifaa vyote vya kujifunzia.
Furaha ya kurudi shule
Ali Musa anafurahi kurudi shule baada ya kipindi kirefu cha kukacha masomo na kwenda kufanya kazi. Anasema:  “Nimerudi shule zaidi ya miezi sita sasa baada ya kutoroka, ambapo nimepokelewa vizuri na walimu na kupata ushirikiano mkubwa.’’
Kauli ya Serikali
Waziri wa Uwezeshaji Wananchi, Wanawake, Vijana na Watoto,  Zainab Omar Mohamed , anakiri kuwepo kwa watoto wanaotumikishwa katika ajira ngumu.
Hata hivyo, anaeleza kuwa  sheria za Zanzibar  na mikataba ya kimataifa inapiga marufuku ajira hizo, ambapo wazazi wanaobainika huchukuliwa hatua za kisheria.
‘’Serikali inapiga marufuku ajira mbaya za watoto zenye madhara, ambazo husababisha wakose fursa mbali mbali ikiwemo elimu. Tupo katika mikakati ya kupinga ajira hizo,’’ anasema Waziri Mohamed.

SOURCE: MWANANCHI.
 
 

Pua inavyomtesa kijana Shabani

Hadithi ya kijana Waziri Shaban inatia simanzi unapoisikia. Ana matatizo makubwa ya kiafya anayohitaji msaada kutoka kwa wasamaria wema.

Dar es Salaam. Uko usemi maarufu usemao: ‘ Hujafa hujaumbika’. Kwa hakika mateso yatokanayo na matatizo ya afya ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Kwa kuwa binadamu hatujui ghaibu, yaani mambo yaliyo nje ya uwezo wa milango yetu ya fahamu, ni vigumu kutabiri hali ya maendeleo ya afya zetu.
Kimsingi, hakuna ajuaye kesho kwani hiyo ni siri ya muumba wa mbingu na ardhi. Dunia ni sawa na kitendawili.
Hadithi ya kijana Waziri Shaban inatia simanzi unapoisikia. Ana matatizo makubwa ya kiafya anayohitaji msaada kutoka kwa wasamaria wema.

Maisha tofauti
Shaban  (28) mkazi wa Gongolamboto, mkoani Dar es Salaam, anaishi maisha tofauti na ya walio wengi duniani. Yeye anapumua kwa kutumia mdomo badala ya pua kama ilivyo ada kwa wanadamu.
Hatua hiyo inatokana na ugonjwa wa nyama za pua anaosema umekuwa ukimtesa kiasi cha kujitokeza hadharani akiomba msaada kwa jamii ili hatimaye aweze kupata tiba na kuondoka na madhila hayo.
Historia ya  ugonjwa huo anasema ilianza Februari 2009, baada ya kuugua mafua makali na koo kuwasha. Alitumia dawa za kawaida bila ya mafanikio.
“Mimi nilijua ni mafua ya kawaida tu lakini kumbe sio,   kwani kila siku zilivyozidi kwenda nilianza kuona pua ikivimba kwa ndani,  jambo ambalo lilinishtua sana,” anasimulia mwanzo wa maradhi yake yanayomtesa hadi leo.
Mwaka 2010 baada ya uvimbe kujitokeza nje ya pua, alilazimika kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Kinyume na matarajio yake, hakupata huduma yoyote mbali ya kuelezwa awe anaripoti hapo kila baada ya miezi mitatu.
Tangu mwaka huo mpaka sasa, Shaban amekuwa akiripoti hospitalini kama anavyoeleza:  “Sikukata tamaa walivyokuwa wakiniambia kurudi kila miezi hiyo bila ya kupewa dawa ya aina yoyote,  hadi waliponiambia kuwa nitoe Sh850,000 ili nifanyiwe upasuaji.”

Ugumu anaoupata
Akizungumza kwa sauti ya mbali na taratibu, huku akitumia mdomo kupumua, anasema maradhi yake yanamweka katika wakati mgumu, kwani anashindwa hata kufanya shughuli za kumpatia riziki.
“Kama unavyojua ndugu yangu, mdomo unafanya kazi mbili; kuongea na kupumua,  hivyo siwezi hata kuongea sana kutokana na hali yangu. Nimeambiwa naweza kupona kama nitafanyiwa upasuaji,’’ anasema na kuongeza:
“ Sina ndugu wa kunisadia kwani nimezunguka sehemu mbalimbali kutafuta fedha lakini nimekosa. Najua Watanzania wenzangu wanaweza kunisaidia na kurejea katika hali yangu ya kawaida.”

Familia yake
Shaban ni baba wa mtoto mmoja. Alioa mwaka 2009 kabla ya kupatwa na maradhi hayo. Alipokuwa mzima alitimiza wajibu wote wa kuhudumia familia akiwa baba na nguzo ya familia. Hivi sasa amegeuka ombaomba, anayezunguka kwa watu wamsitiri maishani.
Anamshukuru mkewe kwa kuendelea kumvumilia hadi leo…“Unajua ukipata matatizo utashangaa kuona mwanamke anakukimbia au anakufanyia unyanyasaji, lakini mke wangu  anaendelea kunitia moyo na kuzunguka huku na huko kutafuta fedha.”
Naye mkewe anayeitwa Anna John,  anasema  hawezi kumkimbia mumewe , kwa kuwa maradhi yake ni sehemu ya majaribu ya maisha yanayoweza kumkumba mtu yeyote.
“Sitomwacha mume wangu nitahangaika naye hadi nihakikishe anapona. Ingawa  sina kazi  nitajitahidi kumtia moyo ili afarijike,’’anaeleza.
Anaamini kuwa kama maradhi hayo yamempata mume wake, yangeweza pia kumpata yeye.  Ni kwa sababu hiyo haoni sababu ya kumtekekeza mzazi mwenzake.
Kwa sasa Ana amekuwa nguzo ya famiia. Anahangaika huku na huko kutafuta chochote kwa ajili ya kuihudumia famila yake ya watu watatu.

SOURCE:MWANANCHI.

Lulu kuweka taarifa za filamu zake kwenye simu

Lulu alisema taarifa hizo zitapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini
Dar es Salaam.
Mwigizaji Bora wa Kike kwa mujibu wa tuzo za Tamasha la Majahazi la mwaka huu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu,  amesema anatarajia kuanza kutoa taarifa zote zinazohusiana na filamu zake kupitia simu za mkononi.
Akizungumza na Mwananchi jana Lulu alisema taarifa hizo zitapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini. “Shabiki wangu pia anaweza kuangalia filamu zangu kupitia mitandao ya kijamii yaani Tigo, Zantel, Vodacom na Airtel. Bado haijawa rasmi hivyo nitakapozindua ndipo nitakapotoa mwongozo halisi,” alisema Lulu.
Kwa mujibu wa Lulu bado hajajua ni lini bidhaa yake hiyo itaanza kurushwa hewani ila kwa sasa yupo katika mazungumzo ya mwisho na wadau wa mitandao ya simu za mikononi.
“Hii ni moja ya mafanikio katika tasnia ya filamu hivyo siwezi nikasema ni lini mpango huu utaanza kurushwa hewani na mashabiki kupata huduma hii, ila natarajia kesho (leo) nitaweza kutoa taarifa rasmi ni lini sasa mashabiki waanze kujiunga na huduma hii.”
Miezi michache iliyopita Lulu alizindua filamu yake mpya Foolish Age katika ukumbi wa Mlimani City, filamu inayofanya vizuri sokoni kwa hivi sasa. Hata hivyo Lulu ni kati ya hazina na vipaji vilivyokuzwa tangu utotoni ambapo anaonyesha kuliteka soko kwa sasa na huenda anaweza kuwapiku wasanii wakubwa wa kike hapo baadaye.
 
 SOURCE: MWANANCHI.

POWER BREAKFAST YAVUMBUA JIWE LINALOCHEZA (NYABUREBHEKA ) UKARA WILAYANI UKEREWE.

 MTARI, KIJANA ALIYE RISISHWA NGUVU YA JIWE HILO LA UKOO.
                                                              MJI WA MWANZA.

NILITOKA MWANZA SIKU YA J3 SAA 3:00 NA MV CLARIUS NI MWENDO WA MASAA MA3 HADI KISIWA CHA NANSIO UKEREWE KISHA NIKAELEKEA BUGORORA ENEO LA KIVUKO KINGINE MWENDO WA DK 20 TOKA NANSIO.

                                     SAFARI KUELEKEA UKARA NA MV NYERERE.

ENEO HILI LA BUGORORA NDIPO KINAPOPATIKANA KIVUKO CHA KUELEKEA KISIWA CHA UKARA MWENDO WA SAA 1.

 MJI WA BWISHA UKARA.
 TOKA BWISHA UKARA SAFARI KWA PIKIPIKI HADI KIJIJI CHA NYANG'OMBE AMBAKO NIKAKUTANA NA KIJIJI CHA MZEE MAKOROKORO. MZEE AMBAYE UMRI WAKE UMEKWENDA MIGUU IMECHOKA AKITEMBEA KWA KUJIVUTA. ANA KIJANA WAKE AITWAE MTARI AMBAYE ALIPOTIMIZA MIAKA 10 ALIRISISHWA KIMILA NGUVU ZA JIWE LA 'BUREBHEKA'.KIJANA SASA ANA UMRI WA MIAKA 20.
 WATU WA MTAA WA DUKE WAKICHEZA KARATA SEBULE KUU.

KIJANA MTARI NDIYE ALIYEKUWA MGENI WETU MIE NA DREVA WANGU WA PIKIPIKI, NAE AKATUTOA PALE NYUMBANI HADI ENEO LA JIWE KWA PIKIPIKI MKAO WA MSHIKAKI (MWENDO WA NUSU SAA).

                                                                MTAA WA DUKE.

TUKAFIKA ENEO LA JIWE LINALOCHEZA NYAMANGA MTAA WA DUKE MTU AMBAYE ALIKUWA MAARUFU HATA WAKAPACHIKA ENEO HILO JINA LAKE (KAMA DAR ES SALAAM VILE MWANANYAMALA KWA HADIJA KOPA).

                                                  HAPA NA PALE MTAA WA DUKE.

MTAA WA DUKE SI MTAA KAMA UNAVYOWEZA KUDHANI KIMJINIMJINI ETI BARABARA, LA-HASHAA! NI ENEO LA UFUKWENI KWA WAVUVI.

 JIWE LA BUREBHEKA LIKO KILIMANI HIVI JUU YA MIAMBA MIKUBWA MASHARTI KABLA YA KULIFIKIA JIWE KTK MLANGO WAKE WA NJIA UNAVUA VIATU UNAVIACHA HAPO, UNAPANDA HADI KWENYE JIWE.
                                                           NJIA KULIFIKIA JIWE.
                                        MTARI AKIWEKA MCHANGA JUU YA FEDHA.

MARA KABAAAAN! JIWE HILI HAPA...TUKAWEKA SH 1000/= KISHA JUU YAKE UKAWEKWA MCHANGA. SHUGHULI IKAANZA KIJANA MTARI (HUKU AKILISUKUMA HIVI KULIZINDUA) AKALIZUNGUMZISHA AKILISIHI KWA LUGHA YA KUKARA KUCHEZA KWANI LIMEPATA WAGENI. DAKIKA KAMA SI SEKUNDE LIKAANZA KUNESA NA LIKAENDELEA ZAIDI NA ZAIDI. SIYO KWAMBA LINA NESA KIUBAVU HAPANA LINA NESA HASWAAA, KUTOKA PEMBE YA FEDHA INAPOWEKWA HADI KULE MBELE KAMA LINAJISUKUMA KUELEKEA ZIWANI. LIKAENDELEA KWA DAKIKA KADHAA KISHA LIKATULIA.

HUKU NIKIBISHA KIMOYOMOYO NAMI NIKAOMBA RUKSA KUJARIBU KULISUKUMA NIKIDHANI KUWA 'SI LINACHEZA KWASABABU KIJANA ANALISUKUMA. ...SUKUMA...SUKUMA... AAAAAH WAPI!! 'NGOMA IMEDINDA' JIWE HALICHEZI NG'O!

                                     UNYAYO WA KAKA YAKE NA NYABUREBHEKA.

SIRI KUBWA YA JIWE LA NYABUREBHEKA KUCHEZA KWA MUJIBU WA MZEE MAKOROKORO ANASEMA KUWA MIAKA YA 1800 (historia haijahifadhiwa vyema) MTU NA KAKA YAKE WALIKUWA KATIKA SAFARI YA KUHAMA KUTOKA KOME UKARA KUELEKEA NYAMANGA MAKAO YAO YA ZAMANI, AMBAPO WALIACHA KUKU NA MBUZI NA MIFUGO MINGINE.(yale maisha ya kuhama hama),SASA KTK SAFARI YA KURUDI MAKAZI YA ZAMANI, MDOGO MTU AKAKANYAGA SEHEMU KWA MGUU WA KUSHOTO AKAPOTEA, KAKAYE AKAFIKA ENEO HILO AKAKANYAGA KWA MGUU WA KULIA HAKUDHURIKA.

KAKA MTU AKAMTAFUTA SANA MDOGO WAKE, KATU ASIPATIKANE. AKAAMUA KUREJEA NYUMBANI KUTOA TAARIFA NAO WAKAFIKA ENEO LA TUKIO, SAKA SANA WASIMPATE KIJANA WAO. HATA SIKU YA 2,YA 3 HADI WIKI, KIJANA KATU ASIONEKANE!

                         UNYAYO WA NYABUREBHEKA KIJANA ALIYEGEUKA JIWE.
                                             KARAI LA KUNYWESHEA MIFUGO.

NDIPO WAKARUDI NYUMBANI KUFANYA TAMBIKO, TAMBIKO LIKAJIBU KUWA KIJANA WAO KAGEUKA JIWE PINDI TU ALIPO KANYAGA ENEO HILO KWA MGUU WA KUSHOTO.
MGANGA AKASEMA HAKUNA JINSI YA KUMREJESHA KIJANA ZAIDI YA WAO (WANANDUGU) KUMTEMBELEA (JIWE BUREBHEKA) KUFANYA TAMBIKO KILA BAADA YA MIAKA 4 KWA KUCHINJA MBUZI MWEUSI WANAYE MKUZA WAO MBUZI ANAYEKWENDA MALISHONI MWENYEWE WAO WAKIMPA HIFADHI YA KULALA TU.

                                                            MIE NA NYABUREBEKA.

INASEMEKANA KIPINDI CHA MIAKA YA NYUMA WAZUNGU WALIFIKA ENEO HILI NA MELI ZAO ZENYE NGUVU WAPATE KUTAFITI KISAYANSI NGUVU HIZO ZA JADI, WAKALIFUNGA MINYORORO NA KULIVUTA KWA MINAJILI YA KULITUPA ZIWANI, WAKACHEMSHA BAADA YA MINYORORO YAO IMARA KUKATIKA.


SOURCE: GSENGO.

AJALI YA HIVI PUNDE YASABABISHA DEREVA WA BODABODA KUPOTEZA MGUU



 TUNAOMBA RADHI SANA WAPENZI WASOMAJI NA WATIZAMAJI KATIKA TAARIFA HII KWA PICHA ZA KUTISHA.

 Dereva wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka sasa (kwani hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu wake wa kulia mara baada ya kugongwa na roli la mchanga katika eneo la daraja  la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa G. Sengo Blog Peter Fabian aliyeweza kuwahi kufika eneo la tukio na kutoa msaada wa gari kumfikisha dereva wa pikipiki hiyo aliyopata ajali Hospitali ya Rufaa ya Bugando, annasema kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Mkolani kuelekea Buhongwa na Roli hilo lilikuwa likitokea Buhongwa kuelekea Mkolani, imetokea wakati dereva wa roli 'akiovateki'  daladala iliyokuwa mbele yake ikibeba abilia, hivyo alipoipita tu daladala hiyo akakutana uso kwa uso na bodaboda.
Baadhi ya bodaboda na wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD Kanda ya Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
 Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.
Sambamba na kuvunjika mguu pia dereva huyo amevunjika vidole vitatu vya mkono wake wa kulia.
NA: PETER FABIAN
SOURCE: GSENGO.

SALHA ISRAEL AITEMBELEA KAMBI YA TANZANIA TOP MODEL 2013.


  Mrembo Salha Israel atembelea kambi ya washiriki wa sindano la Tanzania Top model iliopo katika hoteli ya Jb Belmont iliyopo maeneo ya posta kwa lengo la kuwapa mbinu mbalimbali za kufanya vizuri jukwaani kwani shindano hilo lina upinzani mkali kwa washiriki wenyewe kwa wenyewe.

  Salha alitoa mbinu mbalimbali za kujiamini kwa mwanamitindo awapo jukwaani pamoja na mbinu za kujibu maswali kiusahihi kwa wanahabari ambapo imezoeleka kwa washiriki wengi hushindwa kujibu maswali kiusahihi kitu ambacho hupunguza ari ya shindano.

Washiriki wakimsikiliza kwa makini Salha Israel wakati akiongea nao.
Salha israel mrembo alieng'ara miaka ya 2011 katika mashindano ya urembo nchini,akiongea na washiriki wa Tanzania Top Model 2013 namna ya kujiamini wakiwa katika jukwaa na kujibu maswali endapo watakabiliana na vyombo vya habari.

  Fainali za mashindano haya zitafanyika desemba 7,pia washiriki watapigiwa kura na wananchi ambapo namba maalumu itaolewa hivi punde kumpigia mshiriki umpendae ili kumuongezea alama amabazo zitamwezesha mshiriki wako ashinde.
 
SOURCE:GSENGO.